UTEKELEZAJI BAJETI YA WIZARA YA KILIMO; WAZIRI MKENDA AKUTANA NA BALOZI WA QATAR PAMOJA NA KAIMU BALOZI WA SAUDI ARABIA

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam Miongoni mwa Vipaumbele vilivyoainishwa na Wizara ya Kilimo katika bajeti ya Mwaka 2021/2022 iliyowasilishwa bungeni tarehe 24/25 Mei 2021 ni kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ambao unategemea zaidi mbolea. Katika utekelezaji wake, Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameendelea kukutana na wadau wa makundi mbalimbali,